Dwayne Johnson ndiye actor aliyekunja mkwanja mrefu Hollywood mwaka 2015/2016

Dwayne Johnson

Dwayne Johnson

Mkali wa movie Central Intelligence, ambaye wengi wanamfahamu kupitia series za Fast & Furious, ndiye actor aliyeingiza mkwanja mrefu kuliko wote ndani ya Hollywood na duniani kote kwa msimu wa 2015/2016 akiwa amekusanya kitita cha $64.5 Million sawa na bilioni 138,352,000,000 za madafu. Dwayne maarufu kama The Rock amempita kwa uchache mkali wa Kung-fu mzee mzima Jackie Chan ambaye kwa mwaka uliopita amekuja $61 Milion huku mtu mzima Matt Damon ambaye kwasasa anatamabana filamu yake Jason Bourne akiwa ni muigizaji wa tatu kulipwa hela ndefu kwa mwaka wa jana akiwa na $55 Million.

Kabla ya Dwayne kushika hii nafasi Iron Man actor Robert Downey, Jr alikuwa akishika jackpot ya kulipwa mkwanja mnene. Katika list hii iliyotolewa na Forbes USA inajumuisha wakali wengine Tom Cruise $53 Million na Johnny Depp $48 Million ambao wanashika nafasi ya nne na ya tano.

Orodha ya highest earners pia imetoa shavu kwa Bollywood actor ambaye amekunja mkwanja mrefu kwa mwaka uliopita. Shah Rukh Khan ameingia kwenye list akiwa nafasi ya nane huku kitita chake kikisoma $33 Milion.

Dwayne kabla ya kuibukia Hollywood alikuwa ni mchezaji wa American Football. Ambayo nayo alitupilia mbali na kuibukia kwenye mieleka kabla ya film industry kumpa fursa ambazo hakuwahi kuziwaza.

Comments

comments

Shares