Samatta aipeleka Genk UEFA Europa League

samatta

Its written in the stars far away! waliosema huu msemo hawakukosea. Kama imeandikwa ndivyo itakavyotokea. Mbwana Samatta nyota yake ilishapangwa kung’aa na hicho ndicho kinachotokea kila kukicha. Akiwa mashambuliaji anayejikombea mashabiki kila kukicha nchini Ubelgiji, Samatta ameendelea kufanya kile wanachompendea zaidi, Kufunga magoli pale yanayohitajika the most. Usiku wa jana Samatta akiichezea timu yake ya Genk dhidi ya NK Lokomotiva Zagreb alifunga goli muhimu ndani ya dakika mbili za mwanzo.

Genk ikiwa tayari na matokeo mazuri ya ugenini ilipotoka droo katika mchezo wa kwanza ambapo pia Samatta alitupia goli la pili, waliingia uwanjani wakiwa na nia moja tu kumaliza mchezo mapema. Na kawaida mmalizaji wao tegemezi Mbwana Ally Samatta hakuwaangusha. Ndani ya dakika ya pili Mbwana akafanya yake na kuwapeleka rasmi KRC Genk katika EUFA Europa League.

Kila la heri Samatta, unatuonesha kuwa hakuna kinachoshindikana kwenye nia

 

Comments

comments

Add a Comment

Your email address will not be published.

Shares