Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya, awashinda akina Gareth Bale na Antoine Griezmann

Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya

Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya

Ronaldo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa msimu wa 2016. Ronaldo ambaye alikuwa ashindanishwa na wakali wengine wawili Antoine Griezmann na mshambuliaji mwenzake wa Real Madrid Gareth Bale alionekana ni mshindi wa dhahiri kabla hata ya siku ya tuzo yenyewe.

Rekodi ya Ronaldo kwa msimu huu ambao wengi wanasema ulikuwa msimu mbaya kwake haikuweza kufikiwa na wapinzani wake hao wawili. Ronaldo ni mshindi wa mataji mawili ya makubwa EUFA Euro 2016 akiwa na Portugal na EUFA Champions League akiwa na Real Madrid. Rekodi yake ya ufungaji ilikuwa bora zaidi ambapo yeye ndiye mfungaji bora wa msimu huu wa Champions League akiwa na magoli 16. Ronaldo kwa mwaka huu amefunga jumla ya magoli 51 katika mechi 48 alichozocheza

Akiwa na umri wa 31 Ronaldo ameendelea kupendwa kutokana uwezo anauonesha. Kwa wachezaji wengi wakishafikisha umri huu kiwango hupungua sana. Lakini hiyo ni tofauti kwa Cristiano ambaye ameonekana kuendelea kuimbarika kadiri umri unavyozidi kufika ukingoni.

Matokeo ya kura yalikuwa hivi

Cristiano Ronaldo (Real Madrid/POR) 40
Antoine Griezmann (Atlético Madrid/FRA) 8
Gareth Bale (Real Madrid/WAL) 7

Comments

comments

Add a Comment

Your email address will not be published.

Shares