Lucas Perez straika Arsenal, Mustafi naye kumalizana na Arsenal

Mustafi

Lucas Perez & Shkodran Mustafi

Mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakipambana wenyewe kwa wenyewe takribani wiki mbili sasa toka ligi kuu England ianze. Kama ni mfuatiliaji mzuri wa Arsenal Fan Tv utaona jinsi wanavyogombana hasa linapokuja suala la Wenger In na Wenger Out. Wapenzi wa Wenger hawaamini juu ya kumtimua kocha wao kipenzi kuwa ndo suluhisho la kupata mafanikio ingawa nao wanalalamika kuhusu maendeleo mabovu ya usajili pamoja na sera nzima ya usajili katika club ya Arsenal.

Ijumaa wiki hii, Wenger alifanya mkutano wa waandishi wa habari na kuwapa taarifa ambazo wana Arsenal walikuwa wakizisubiria. Beki mahiri wa Ujerumani Shkodran Mustafi ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal toka dirisha lilipofunguliwa sasa yuko tayari kusaini. Kwa mujibu wa Wenger, dili ya Mustafi imekwisha kwa asilimia 99%. Kwa kawaida Wenger akisema 99% huwa anamaanisha dili imekwisha ila anasubiri muda muafaka kumtangaza mchezaji wake mpya. Hapo mwanzo Valencia CF walikataa kumuuza Mustafi kwa dau lolote chini ya Pound milion 50. Hali hiyo ilimfanya Wenger kwenda mwenyewe Spain kufanya makubaliano, na taarifa aliyotoa jana ina maana mwana uchumi Wenger alifanikiwa kuwashusha maana kwasasa Mustafi ana price tag ya  Milioni 35 pound.

Wapenzi wa Arsenal  pia walipewa habari nzuri iliyojibu kilio chao cha muda mrefu. Mashabiki wa Arsenal siku zote walikuwa wakitaka straika anayejielewa na si yule anayetumia muda mwingi saluni kutengeneza nywele. Mzee Wenger ambaye katika mkutano wa jana alionekana mwenye kujiamini aliweka wazi kuwa straika waliyekuwa wakimtafuta wamekaribia kumpata.  Arsenal imefikia dau la milioni 20 Euro lililowekwa na  Deportivo La Coruna ili kumpata mkali wao wa magoli  Lucas Perez. Wenger alidai uhamisho wa Perez uko ukingoni na kwamba wanatarajia kumfanyia vipimo wikiendi hii kuanzia Ijumaa. Kwa msimu huu uliopita Lucas Perez  amefunga magoli 17 katika mechi 37.

Angalia mambo ya Lucas Perez hapa chini

Comments

comments

Shares