Tiggs Da Author ni mwanamuziki wa Tanzania anayefanya vizuri England. Kwanini tunampotezea

Tiggs Da Author

Tiggs Da Author

Niliwahi kuandika kuhusu mastaa wa Tanzania na wanaofanya vizuri nje ya Afrika. Watu wachache walicomment wakidai kuwa mastaa hao wamekimbia nyumbani. Which for me wasn’t a reason. Nadhani tunaandamwa na tatizo la ubaguzi wa kifikra. Tunadhani Mtanzania aliye nje ya nchi hapaswi kuitwa Mtanzania. Na hii imetokea hata kwenye katiba mpya tuliyoipendekeza, kwasababu wanazojua wao wanasiasa wakalitupilia mbali wazo la uraia pacha.

Leo nimeamua kuandika tena kuhusu Tiggs Da Author maana hata kama watu hawataki huyu jamaa anafanya vizuri na anahitaji support yetu. Nilipokuwa ughaibuni (UK) mwezi uliopita nilikuwa nikizisikia nyimbo za Tiggs Da Author redioni.  Tiggs Da Author amekuwa akipata airtime ya kutosha na moja ngoma zake zinazosumbua kwasasa Uingereza inaitwa RUN aliyomshirikisha Lady Leshurr. Ngoma iliyompatia umaarufu mkubwa inajulikana kwa jina la Georgia

Inawezekana kabisa Tiggs anafanya muziki kwa lugha tofauti ambao wengi wanaweza wasiilewe but kama tunaweza kusupport mziki wa Nigeria sidhani kama lugha anayotumia ni tatizo ya kukubaliwa nyumbani. Najua kuwa wengi tunakataa kiingereza na ndio maana hata Mayunga amepewa support ndogo sana. Lakini kiukweli hatuna sababu nyingine ya kuwakataa watanzania ambao hawatumii Kiswahili katika ngoma zao.

Angalia ngoma na performance zake hapa chini

Comments

comments

Shares