Finally, Arsenal yamtangaza Lucas Perez kuwa straika wao Mpya

Lucas Perez

Lucas Perez, Klabu ya Arsenal jioni ya leo imemtangaza rasmi Lucas Perez kuwa mchezaji wao. Perez ambaye aliingia kwenye rada ya Wenger baada Vardy kuichomolea Arsenal alifanyiwa vipimo siku ya Jumamosi na leo kutangazwa rasmi baada ya documents zote kukamilika. Usajili wa Lucas umekuwa na mitazamo miwili tofauti kwa mashabiki wa Arsenal ambapo wengine wanasema ni panic buy wakati wengi wanaamini alikuwa chaguo la pili la Wenger kwa muda mrefu.

Wanaodai ni panic buy wanamuona Wenger ni kama kocha aliyefeli kwenye dirisha la usajili na kwamba suala la kununua haraka haraka dakika za mwisho lilitokana na shinikizo la mashabiki. Hatahivyo, mashabiki wanaokubaliana na usajili huu wanasema ni bora kuleta mchezaji atakayeleta upinzani kwa Giroud kuliko kutoleta kabisa. Hata kama Perez hatofanikiwa itatosha kumuonesha Giroud kuwa yeye si straika peke yake ndani ya Arsenal.

Kwa baadhi ya mashabiki ambao hawafungamani na upande wowote wanasema wako tayari kwa mabadiliko. Kama Lucas Perez ataleta mabadiliko kwenye safu ushambuliaji wao hawana tatizo hata kama mchezaji huyo wamemjua juzi tu kwenye Youtube.

Comments

comments

Shares