jah prayzah ft diamond platnumz yapata viewers milioni 1 ndani ya wiki mbili mwenyewe afanya party. (Video)

jah prayzah ft diamond platnumz

Jah Prayzah ft Diamond Platnumz

Kuna wakati huwa najiuliza hivi inaweza kupita wiki bila ya Diamond Platnumz kuwa midomoni mwetu? kama sio nyumbani Tanzania atakapotengeneza headline basi nje ya nchi. Jah Prayzah mwanamuziki toka Zimbabwe amevunja rekodi yake binafsi kwa kufikisha viewers milioni 1 ndani ya wiki mbili.

Unajua kwanini?

Well, panapo ushiriki wa Diamond Platnumz ‘Simba’ , ama LION OF AFRICA kama huko Zimbabwe walivyoamua kumuita, tegemea hilo kutokea. Ngoma ya Watora Mari ya Jah Prayzah iliyotengenezwa ndani ya Wasafi Records huku Diamond Platnumz akiingiza mautundu yake ndio sababu hasa ya Jah Prayzah kuandika hivi  kwenye instagram

“Thanks to all my fans out there,watora mari video with @diamondplatnumz has just reached a million views in a space of 2 weeks”

Najua haterz wa Diamond Platnumz watakana but hii sio mara ya kwanza kwa Simba kuwanyanyua wasanii wenzake kupitia mitandao ya kijamii. Kwa mfano kaka mkubwa AY pamoja umaarufu na ubora alionao hakuwahi kufikisha milioni moja katika Youtube katika maisha yake ya muziki. Lakini leo hii tunazungumzia milioni 7 na laki mbili views katika Youtube kupitia ZIGO Remix aliyofanya na Diamond Platnumz. AKA toka South Africa naye alishasema isingekuwa Diamond Platnumz, fan base yake kwenye social media isingekuwa kwa ghafla kiasi kile

So does it mean kwamba Diamond ndo msanii anayetafutwa sana mitandaoni kwa upande wa East Africa? Well, ni lazima tuwe wakweli jibu lake hapo ni YES. Diamond Platnumz ndiye King wa Social Media. Uwe unakubali au unakataa haitakusaidia kitu.

Juzi tu YCEE ametoka kusema kule kwao Nigeria, Kidogo ya Diamond inapigwa pengine kila baada ya dakika 20. Kwanini sasa asisumbue kwenye social media kama Simba ana fan base mpaka magharibi.

Wimbo wa Jah Prayzah sasa utaanza kurushwa MTV Base kuanzia leo.

Hongera sana Jah Prayzah umefanya vizuri kuja kushirikiana na Simba aka Diamond Platnumz baba mzazi wa Tiffah

Hii video ya hapa chini utawaona  wenyewe akina Jah Prayzah walivyo na furaha huku wakimshukuru Diamond Platnumz kwa kufanikisha ndoto yao

Na hii ndo ngoma yenyewe iliyowatoa kimasomaso ambayo ndiyo wanayomshukuria Diamond Platnumz

Comments

comments

Shares