Joe Hart akosa namba Man City, Apelekwa Torino kwa mkopo

Joe Hart

Joe Hart, kama ni bahati mbaya za msimu mpya basi hii ya Joe Hart itakuwa bahati mbaya kuliko zote. Joe Hart ameshindwa kuhakikishiwa namba na kocha mpya wa Manchester City, Pep Guardiola. Wengi hawakuliona hili likitokea hasa kutokana na umahiri alionao golini kipa huyo namba wa England.

Manchester City italazimika kuchangia mshahara wa Joe Hart kipindi msimu mzima atakapokuwa Torino klabu iliyokubali kumfichia aibu ya benchi mlinda mlango huyo. Mshahara wa Joe Hart ni Pound 135,000 kwa wiki. Klabu ya Torino iko tayari kumchukua muda kwa mkopo endapo tu City watachangia kiasi walichopendekeza.

Mkopo mwingine wa kushangaza umetokea Arsenal ambapo Joel Campbell ambaye alionekana kuanza kujidhatiti katika kikosi cha kwanza alipoamua kumuomba Wenger aondoke kwa mkopo ili akapate nafasi ya kucheza mara kwa mara. Campbell amejiunga na Sporting Lisbon, Ureno na tayari ameanza kuichezea timu hiyo. Wikiendi iliyopita aliingia dakika ya 69 katika mchezo dhidi ya Porto ambapo Sporting Lisbon ilishinda 2-1

Comments

comments

Shares