Yametimia. Shkodran Mustafi Arsenal rasmi

Shkodran Mustafi Arsenal

Mustafi Arsenal

Masaa matatu ya jioni ya Jumanne yatakuwa yakukumbukwa kwa muda kwa takribani miezi kadhaa ijayo. Sio kwasababu Arsenal wamevunja rekodi ya wachezaji ghali hapana. Ni kwasababu this time, Wenger ameamua kufanya usajili wa kueleweka kwenye kikosi chake.

Shkodran Mustafi beki mahiri toka Valencia na mwenye namba ya kudumu kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani amedondoka wino rasmi. Hatamaye Wenger kwa mara ya kwanza katika historia ya utawala wake ametumia zaidi ya milioni 80 katika msimu mmoja kufanya usajili. Hii haitowatoka mashabiki wa Arsenal kwa miaka mingi ijayo hasa ukizingatia ubahiri na ubovu wa Transfer Policy ya Arsenal.

Mustafi anakuja kuongeza nguvu na kwa mara ya kwanza toka mwaka 2003 kikosi cha Arsenal kinanza kuonekana cha ushindani. Mustafi anaongozeka kwenye list ya mabeki mahiri wakiongozwa na Koscielny, Monreal, Mertesacker, Paulista, Bellerin, Debuchy, Gabriel, Gibbs na Rob Holding.

Wenger kwa miaka mingi hakuwahi kuwa na machaguo katika safu yake ulinzi iliyoonekana kuwa dhaifu kiasi cha kutundikwa mabao nane na Manchester United 2011, na mabao sita walipocheza na Chelsea miaka miwili baadae.

Comments

comments

Shares