Black Eyed Peas warudia “Where’s The Love”. Mastaa kibao washiriki

Where's The Love- Black Eyed Peas

Kundi la The Black Eyed Peas linaongozwa na Will.I.Am limeurudia wimbo wao maarufu “Where’s The Love” ambao ulilenga kufanya harakati za kusambaza upendo duniani. Original version ya wimbo huo ulichukua tuzo kadhaa na walimshirikisha mtu mzima Justin Timberlake katika chorus na bridge.

Safari hii, remix ya wimbo umekusanya mastaa zaidi ya thelathini ukiwa na lengo moja tu kuieleza dunia umuhimu wa upendo ambao kwa kiasi kikubwa umetoweka. Katika wimbo huu remix ulioziachiwa mtandaoni Sept 1, 2015, The Black Eyed Peas wametumia footage na picha mbalimbali za matukio ya kweli ya kinyama yanayoendelea duniani. Kuna picha ya mtoto aliyefariki baharini baada ya ubalozi wa Canada kumyima visa yeye familia yake wakati wakikimbia mapigano na utawala wa ISIS huko Syria. Katika verse ya P.Didy utaona vita kati ya polisi na Wamarekani weusi ambayo imekuwa ikishika headline katika miaka ya hivi karibuni.

So I let see the videos (hii mpya na ile ya zamani) upate kuona kinachoelezewa ndani yake.

Where’s the Love, Remix

Where’s the Love, Old version (orginal version)

Comments

comments

Shares