Ni pale KR Muller anapozidiwa na mitungi

KR Muller

Wasanii wengi wa Bongo wanashutumiwa kwa kuendekeza kinywaji. Na tukio la hivi karibuni la msanii mkongwe toka TMK, KR Muller ndo limezidisha shutuma za ulevi dhidi ya wasanii hao. KR Muller ambaye alihama kundi la Wanaume Halisi na kwenda Rada ya TID mwanzoni mwa mwaka huu, alijikuta akikutana na aibu ya mwaka baada ya kuzindiwa na kinywaji. Ingawa yeye mwenyewe anadai si tukio la kushangaza maana suala la kuzidiwa na kilevi hutokea kwa watu wengi tu.

Juma Nature kiongozi wa TMK Wanaume Halisi alikaririwa akisema kuwa toka KR ahamie kwa TID tabia yake imebadilika sana. Kitu ambacho kimetafsiriwa kama ni shutuma dhidi ya kiongozi huyo mpya wa KR Muller. Hata hivyo KR mwenyewe alikuja kukanusha taarifa hizo na kusema kuhamia kwa TID ni jambo zuri kimaendeleo yake ya muziki na hakuna suala la kuharibikiwa kama ilivyotamkwa awali na Juma Nature.

Comments

comments

Shares