“SALOME” YA DIAMOND GUMZO. HATERZ WADAI KAIBA, UONGOZI WAWEKA WAZI KIBALI

Diamond Platnumz akipewa mikataba ya kutumia wimbo wa Salome
Diamond Platnumz akiwa na uongozi wa Saida Karoli wakati wa kusaini makubaliano ya kutumia wimbo wa Saida Karoli.

Haters wa Diamond Platnumz will never stop hating kwasababu hiyo ndo kazi yao. So kila kukicha huamkia kwenye social media za Simba ili wapate kitu cha kuchukia kwa siku hiyo. Tafiti zisizo rasmi zinaonesha kuwa hawa haters ndo chanzo kikubwa cha Diamond Platnumz kufanya vizuri kwasababu kwa ku-hate kwao wamekuwa wakimpa promo kubwa mitandaoni.

This week, Dimaond Platnumz ametupa bonge la ngoma SALOME akiwa ametumia kazi ya mwanamuziki mkongwe Saida Karoli. Muda mfupi tu baada ya ngoma kutoka, haters wakavamia mitandao ya kijamii na kuifanya ngoma kufanya vizuri ndani ya muda mfupi.

Haters walianza kama kawaida yao kwa kumtukana. Kisha wakaendelea kusema ngoma imejaa matusi. Lakini hawakuishia hapo. Wakasema eti Simba KAIBA NGOMA YA KAROLI. Kwa binadamu mwelevu atajua wazi msanii wa kimataifa level za Diamond Platnumz hawawezi kuiba ngoma. Nilizishangaa hizo shutuma na pia nikajiuliza kama uongozi wa Diamond Platnumz unaweza kuwafikia akina NE-YO utashindwaje kumfikia Saida ambaye ni Mtanzania mwenzetu?

Well, kumbe hizi shutuma zimefika mbali na uongozi wa Simba Dangote ukaamua kutoa ufafanuzi. Sallam mmoja wa mameneja wa Diamond akaandika ujumbe huu kwenye wall yake

“Tunakushukuru sana Uongozi wa Saida Karoli Mzee Felician Mutakyawa kutupa Haki Na Baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome. Tunatambua kwamba Nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania. #Salome Link in @diamondplatnumz & @rayvanny’s Bio”

Bila shaka Sallam na wenzake nao walikuwa wameshtushwa na hizi shutuma wakaamua kuwaonesha haters kuwa wao wamejipanga kwa kila kitu wanachofanya.

Comments

comments

Shares