Jim Carrey ashitakiwa kwa kusababisha kifo cha mpenzi wake wa zamani

jim carrey

Mkali wa comedy huko Hollywood Jim Carrey, 54, ameingia katika matatizo na mamlaka ya Los Angeles baada ya kifo cha aliyekuwa mpenzi wake kuhusishwa na matumizi ya dawa ambazo alikuwa akimpa. Kifo cha Cathriona White ambaye pia ni muigizaji nchini Marekani mwenye asili yaIreland, kimetokana na kuzidisha matumizi ya dawa alizokuwa akizipata toka Carrey.

Mark Burton, mume wa White, amesema hatoweza kuvumilia kuona mkewe akikosa kutendewa haki. Kifo cha Cathriona kilitokea mwaka jana na Jim Carrey anatuhumiwa kumpa dawa hizo ingawa alikuwa anajua White alikuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo (depression). White alijizidishia dawa kwa makusudi ili kuondoa uhai wake.

Jim Carrey, ambaye umaarufu wake umetokana na mafanikio makubwa ya filamu yake ya The Mask, anasemekana kuzipata dawa hizo kupitia jina la uongo la Arthur King na alikuwa akimpeleka White kila alipozihitaji. Jim na Cathriona walikuwa wapenzi kwa muda mrefu na kila walipoachana walikuwa wakirudiana. Hata ilipotokea White kuolewa na Mark wawili hao hawakuachana kuwa marafiki.

the-mask

Comments

comments

Shares