Kilimanjaro Queens yanyakua ubingwa wa CECAFA Chalenji huko Jinja, Uganda

the-kili-quens2

The Kilimanjaro Queens wakicheza ugenini katika mashindano ya kihistoria ya CECAFA Challenge wamefanikiwa kutwaa ubingwa kwa kuichabanga Kenya maarufu kama Harambe Starlets kwa mabao 2-1. Katika mchezo huo uliofanyika Jinja, Uganda Kilimanjaro Queens ilipata magoli yake yote kupitia kwa Mwahamisi Omar dk 28, 45.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Alfred Lucas, mashujaa wetu wataondoka leo kurudi nyumbani Dar es Salaam, lakini watapitia kwanza Kagera kutoa pole kwa wahanga wa tetemeko la ardhi kisha watarejea jijini siku ya kesho.

Comments

comments

Shares