Ndege ya Air Tanzania yatua. Ni ndogo lakini asante Rais Magufuli kwa kuthubutu

air-tanzania

Shirika la ndege la Tanzania limekuwa mkiwa kwa miaka sana. Likijiendesha kwa hasara kwa kipindi kirefu sana na yote hiyo ilitokana na ubadhilifu wa mali za shirika hilo. Rais Magufuli kwa kutambua umuhimu wa ATCL katika kuchangia uchumi na kukuza utalii ameamua kulipa nguvu shirika hili kwa vitendo ili lianze rasmi kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Tunafahamu watu wengi wamekatishwa tamaa na ATCL na wengine wakibeza ununuzi wa ndege hizo ambazo ukizilinganisha na wenzetu wa Kenya, Ethiopia ama Rwanda ni ndogo. Lakini kwa mwerevu anapaswa kumpa pongezi Rais kwa kuthubutu. Tumeshuhudia kwa miaka mingi shirika hili likianguka siku baada ya siku, kupewa ndege kama hizi mbili ni hatua nzuri kwa ustawi.

air-tanzania2

Hivyo basi, badala ya kulalamika mitandaoni kuwa serikali imenunua ndege ndogo ni vyema tukapongeza hatua hiyo hasa ikizingatiwa ilikuwa ikihitaji utayari wa serikali kufanya hivyo. Na serikali ya Magufuli imeonesha utayari.

Hongera ATCL kwa kupata ndege, umakini katika utendaji sasa unahitajika.

Comments

comments

Shares