Mjengo mpya wa Diamond na Zari huko South huu hapa. Simba atoa ujumbe mzito unaomlenga ex wa Zari

nyumba
Katika hali inayoonesha kukaraishwa na maneno ya kejeli anayotupia mtandaoni Diamond Platnumz ameamua kutuonesha mjengo mpya alionunua kwaajili ya Zari huko South Afrika na maalumu kwaajili ya familia yake. Timu pinzani zinazomkataa Zari na zile zinazomponda Diamond Platnumz kwamba hana mkwanja zikiongozwa na ex husband wa Zari wamekuwa wakimtukana pamoja na kumuita masikini aliyejawa na shida. Kitu ambacho kimekuwa kikimuumiza Diamond Platnumz.

nyumba3

Hali hii ya matusi imemfanya Diamond Platnumz kuonesha nyumba aliyonunua kwaajili ya mama mtoto wake huko South Africa.

Huu hapa chini ni ujumbe alioutoa Simba ambao unasemekana umemlenga Ssemwanga ambaye ni mume wa zamani wa Zari ambaye ndiye hasa aliyeanzisha uvumi kwamba Diamond Platnumz hana mkwanja anaosemekana anao. Katika ujumbe huu Simba anamchana kwa kumwambia kwamba jamaa anazuga ana mkwanja wakati watoto wake wanaishi nyumba ya kupanga na kwamba nyumba alimnunulia Zari watoto wa jamaa nao wanakaribishwa kukaa.

“They are busy bragging them selves that they are Rich while their Kids staying in the Renting House… and today a person they are daily abuse and saying that he’s broke Bought a House, so that their Kids can have a better life as their dad always wish on Social Media….. Happy Birthday Mama tee i hope you like our new South African House….Can’t wait for your Big weekend in Zanzibar tomorrow....I love you So much mama tee, we ndio Salome wa Moyo wangu pekee @zarithebosslady 😙🌷🎉🎂🎂🎉🌷 (Wanakazana kujisifu Matajiri Ilhali watoto zao wanaishi kwenye Nyumba zakupanga… halaf leo yuleyule wanaemtukana kutwa kwenye Mitandao kuwa Masikini, kajawa na shida, Kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi Maisha bora kama wanayoyatamani… Heri ya siku ya Kuzaliwa Mama tee wangu…. Nakupenda sana na unalifahamu hilo…natumai umeipenda Nyumba yetu hii mpya South Africa… nasubiria kwa hamu kusheherekea nawe siku yako hii kubwa kesho zanzibar….😙🌷🎉🎂🎂🎉🌷)”

Comments

comments

Shares