Kwanini Ali Kiba alizimiwa Mic show ya Chris Brown Mombasa?. Meneja wa Diamond aonekana backstage wakati mic inazimwa

alikibatz

Kuna vitu huwa vinaleta picha mbaya kwenye game yetu ya muziki wa Tanzania. Tukio la kuzimiwa microphone alilokutana nalo Ali Kiba huko Mombasa wakati wa show ya Chris Brown limeibua maswali mengi kuhusu sababu za meneja wa Diamond Platnumz kuwa back stage wakati wa tukio hilo.

Kiba mwenyewe anadai hajafurahishwa na kitendo cha Sallam kwenda backstage wakati show ilikuwa haimuhusu. Ingawa Ali Kiba amesisitiza hana bifu na Diamond Platnumz lakini pia amesema hakufurahishwa na kitendo cha meneja huyo kwenda backstage kitu ambacho kwa watu kinaweza kutafsiriwa kama ndo sababu ya Ali Kiba kuzimiwa mic.

Anyway, whatever happened hatuwezi kuujua ukweli ila si tukio zuri kumkuta msanii mkubwa kama Ali Kiba. Pole sana King Kiba matukio kama hayo huwa tunafanyia uchochoroni huku. Lakini pia tumpongeze kiba kwa kuonesha umahiri aliporudi tena jukwaani na kugonga show kama hakuna tukio lililomkuta.

Angalia mahojiano aliyofanya na Mseto kujua kilichojiri siku ya tukio

Comments

comments

Shares