Kumuona Diamond Platnumz na Ne-Yo London ni Pound 63

Diamond Platnumz na Neyo

Diamond Platnumz na Neyo watakuwa na tour ya pamoja nchini Uingereza kuanzia tarehe 7December mpaka tarehe 16 December. Show zote za wakali hawa zitaanzia Glasgow na kumalizia O2 Academy Brixton, London.

Diamond Platnumz na Neyo wamekuwa karibu toka walivyokutana kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini na kuanzia hapo mbali ya kuwa wafanyabiashara wanaojuana wamekuwa marafiki.

Wakati natafuta ticket ya kwenda kuona show ya tarehe 16 December nilishtushwa kidogo na ugharama wa bei. Kwa kawaida bei huwa zina range kati ya pound 20 mpaka 40 hivi. But kwa hii show ya London ambayo inafanyika kwenye stage kubwa ambayo nina hakika itakuwa tofauti na stage nyingi alizowahi kupanda Simba, show itagharimu pound 63 hivi sawa na laki na sabini hivi za kibongo. Kwa wabongo walioko huku ughaibuni najua watakuwa wanakimbizana na kazi za mwingireza sasa  ili waweze kumuona kijana wao. Kila la heri Diamond, endelea kuturushia bendera yetu vizuri

Comments

comments

Shares