Tiggs Da Author aendelea kuitangaza Tanzania kupitia muziki wake Ulaya

Tiggs Da Author ni Mtanzania

What I like about Tiggs Da Author ni kwamba hajifichi asili yake. Pamoja na mafanikio anayoyapata katika tasnia ya muziki nchini Uingereza na Ulaya kwa ujumla, Tiggs amekuwa mwepesi kuweka wazi asili yake na lugha yake ya kwanza kuzungumza. Ingawa Tiggs Da Author si peke yake mwenye asili ya Tanzania anayefanya vizuri England, maana yuko pia Ady Suleimani ambaye baba yake ni Mzanzibar, Tiggs amekuwa amekuwa wa kipekee kutokana na kutosahau lugha yake ya kiswahili pamoja na kuondoka Tanzania akiwa na mdogo.

Hivi karibuni wakati akifanya interview na Spindle Magazine pamoja na kuzungumzia muziki wake, pia alifurahishwa na uwezo wa interviewer ambaye alisema maneno machache ya Kiswahili. Kwa Tiggs, ambaye EuroNews wanamfananisha na Pharrell wa Ulaya,  Tanzania iko moyoni. Post zake nyingi amekuwa akiweka na bendera ya Tanzania kuonesha kuwa popote aendako duniani na mafanikio yoyote ayapatayo kupitia muziki huko Ulaya bado ataendelea kujivunia Tanzania.

Hii hapa chini ni ngoma yake mpya Swear Down aliyomshirikisha Yungen.

Angalia interview yake na Spindle hapa chini

Comments

comments

Shares