RONALDO AZIDI KUMNYANYASA MESSI, ASHINDA FIFA Men’s Player Award 2016, TUZO YA PILI KWA 2016 BAADA YA BALLON D’OR

Ronaldo ametangazwa mshindi wa tuzo za kwanza za FIFA baada ya FIFA kutengana na tuzo ya Ballon d’OR  ambayo pia Cristiano aliichukua Dec 12, 2016 ikiwa ni ya nne kwake. Katika tuzo hizi mpya Ronaldo ameshinda kipengele cha mchezaji bora wa kiume wa FIFA kwa mwaka 2016 (FIFA Men’s Player Award 2016).

Hii inakuwa ni tuzo ya pili kubwa kuchukuliwa na Ronaldo ndani ya mwaka 2016. Mwaka 2016 umekuwa bora kwa CR7 baada ya kuisaidia Real Madrid kuchukua ubingwa wa Champions League na pia kuiwezesha timu yake ya taifa kuchukua ubingwa wa EURO 2016.

Wiki iliyopita Real Madrid iliwaalika wachezaji wake waliowahi kuchukua Ballon d’Or ili kuhudhuria sherehe ya kuziweka wazi tuzo za Ronaldo ambazo kuanzia mwaka 2017 hazitakuwa tena chini ya FIFA baada ya shirikisho hilo kuanzisha tuzo zake peke yake. Wachezaji walioalikwa walikuwa Michael aliyeshinda 2001, Luis Figo, Zidan, na Ronaldo de Lima.

Vipengele vyote vya tuzo za FIFA ni kama ifuatavyo#

Mchezaji Bora wa Kiume 2016
Cristiano Ronaldo: 34.54% za kura zote
Lionel Messi: 26.42%
Antoine Griezmann: 7.53%

Mchezaji Bora wa Kike 2016
Carli Lloyd: 20.68% za kura
Marta: 16.60%
Melanie Behringer: 12.34%

Kocha Bora Timu za Wanaume 2016


Claudio Ranieri: 22.6% za kura zote
Zinédine Zidane: 16.56%
Fernando Santos: 16.24%

Kocha Bora Timu za Wanawake 2016
Silvia Neid: 29.99% za kura zote
Jill Ellis: 16.68%
Pia Sundhage: 16.47%

Puskas Award (Goli Bora la Msimu)

Mohd Faiz Subri: 59.46% za kura zote
Marlone: 22.86%
Daniuska Rodriguez: 10.01%
Wengine: 7.68%

Mashabiki Bora wa Msimu
Mashabiki wa Borussia Dortmund na Liverpool: 45.92% za kura zote
Mashabiki wa Iceland: 31.37%
Mashabiki wa ADO Den Haag: 22.71%

Kwa ambao hawafai mashabiki wa Liverpool na Borussia Dortmund wameshinda tuzo hii kutokana ushabiki wa kizalendo ambao wote kwa pamoja waliimba na kushangilia kwa kutumia wimbo wa timu ya Liverpool YOU WILL NEVER WALK ALONE. Kitendo ambacho ni nadra kutokea wakati timu zinaposhindana.

Tuzo ya Uungwana (Fair Play)
Atletico Nacional- Colombia

Kikosi cha Msimu cha FIFA

Comments

comments

Shares