Diamond Platnumz ajitetea kwa Gwajima. Ni baada ya kumtaja kwenye wimbo wake

Haya mambo nyie yaacheni tu kama yaliyo. So hiki ndicho kilichotokea. Diamond Platnumz kaachia ngoma “Acha Nikae Kimya” ambayo ndani yake kazungumzia mambo mengi yanayoendelea sasa hivi. Ngoma imejaa tungo tata huku kila mtu akitafsiri kivyake. Wapo waliona hiyo ngoma imetungwa kuwatisha watu hasa wasanii wengine, wapo wengine wanaodhani ndani hii ngoma hakuna aliyenusurika, wote wamechanwa.

Kuna watu wamedai haiwezekani Roma apotee muda mfupi tu halafu ngoma ya Diamond itoke huku ikiwa na jina la Roma ndani. Watu hao hao mitandaoni wakahoji kawezaje kutunga kwa haraka kiasi hicho na kuachia ngoma iliyofanyiwa mixing kabisa. Kwa utashi wangu mdogo sioni kama hilo ni tatizo. Kwani nimepata kuwaona akina Joh Makini wakiandika ngoma studio ndani masaa ya mawili imekwisha na zikaja kuwa hits kila sehemu. Ni uwezo tu wa uandishi ukichanganya na uwezo wa producer.

Anyway, ishu ya mezani hapa ni kauli ya Diamond Platnumz kujitetea kwa Askofu Gwajima. Kuna picha ya Gwajima (meme) imekuwa ikitambaa mitandaoni ikiwa na maneno ambayo yanasomeka kama onyo ama kitisho kwa Diamond Platnumz.

Bwana mdogo baada kuona askofu povu limemtoka akaona isiwe shida akakimbilia kwenye eneo lake la kujidai, sisi tunaitaga Instagram akatupia bonge la message la kujitetea asigeuzwe maji kesho…hahaha patamu hapo. Anyway, kitendo cha kutaka suluhu ni cha kiungwana ingawa sijaona akiomba msamaha vizuri. Kama Chibu anaona hajaeleweka vizuri ni vyema aende kanisani kwake kesho akazungumze naye.

Mbali ya sakata hilo, sidhani kama mashairi ya huu wimbo yanambeba Konda kama inavyosemekana maana kama hilo ndo lengo lake basi uandishi ni mbovu coz ni wazi Konda naye kachanwa kimtindo.

Comments

comments

Shares