Diamond Platnumz amlilia Roma kwenye wimbo uliojaa utata.. “Acha Nikae Kimya”

Roma Atekwa, Diamond Platnumz- Acha Nikae Kimya

Haya yanachoendelea Tanzania kwa sasa Mungu pekee ndo anajua yatakapotufikisha. Ila tukiwa kama binadamu woga umeanza kutujaa kwenye mioyo yetu. Tunajua wapo watu wenye nia mbaya na taifa letu. Tusipokumbushana amani tuliyonayo sasa, tutaililia ikipotea.

Yuko Wapi Roma na wenzake? wamefanya nini hasa? Haya maswali mpaka sasa hayana majibu. Je wametekwa kutengeneza woga miongoni mwa outspoken people, hasa Roma? Nani aliyewateka? Vyombo vya usalama vimeingia kazini kuwatafuta but endapo wakipatikana tunapenda kujua aliyewateka. Ikiwezekana waliowateka wachukuliwe hatua.

Diamond Platnumz, taswira ya muziki wetu, ndani na nje ya Tanzania, ameamua kutoa kilio chake kupitia wimbo ambao kwa hakika unaweza kukutoa machozi. ACHA NIKAE KIMYA ndio jina la wimbo. Alichokizungumza Diamond Platnumz ndani ya hii ngoma ni zaidi ya upoteaji wa #Roma. Wimbo huu unaonesha kilicho ndani ya mioyo ya watanzania– #WOGA NA MKANGANYIKO WA MAWAZO. Hakuna anayejua taifa letu nini kitatokea kesho.

Roma ni baba wa familia. Mke na mtoto wanamuhitaji. Watanzania tunamuhitaji, wapenda burudani tunamuhitaji, na mashabiki wake wanamuhitaji.

#Nakupenda_Tanzania.

ACHA NIKAE KIMYA -DIAMOND PLATNUMZ . To download this song tembelea Wasafi.com

 

Comments

comments

Shares