Wape – Bongolos ft Asteria (video). Majani tunakumiss sana

WAPE, ngoma toka kwa kundi la Bongolos ni ngoma inayotupa ladha ambayo kwa muda sasa tumekuwa tunaikosa. Ladha inayotokana na midundo iliyosimamia ukucha, kwa ufupi ukimya wa Majani ulisababisha baadhi ya wapenzi wa Hiphop kubadili uelekeo na kuhamia kwingine. Na kama wewe ni miongoni mwa wale waliokimbia real hiphop kwasababu tu midundo ya ajabu ilikuwa imekosekana, now its your time to come back. Wasilikilize #Bongolos walivyoutendea haki huu mkono.

Majani shikamoo zako genge. Tuseme tu ukweli ukimya wako P-Majani unatunyima burudani. Kwenye mkono wa Majani hata kama ulikuwa hujui utajua tu..

Comments

comments

Shares