Rais Magufuli amfagilia David Kafulila ziarani Kigoma

Rais Magufuli amfagilia David Kafulila ziarani Kigoma

Wakati mwingine huwa tunawaza kwanini mashujaa wa nchi hii huwa wanadharauliwa. Imetuchukua muda mrefu kumpata kiongozi ambaye yuko tayari kusifia kazi nzuri inayoleta tija kwa taifa. Wakati David Kafulila akiibua sakata la IPTL na ESCROW viongozi wengi wenye nyazifa zao walimkejeli na kumtaka afung mdomo. Leo hii tumepata kiongozi mkuu wa nchi ambaye yuko tayari kuzitambua juhudi za Kafulila na pia kutamka hadharani. Kwa hili kwa hakika lazima tumpongeze Rais Magufuli.

Kauli ya kutambua jitihada za David itawahamasisha wanaharakati wengine ambao kipindi cha nyuma walikuwa wakidharaulika na kuonekana vimbelembele. Asante sana Kafulila, now kazi yako na uzalendo wako unaonekana katika jamii.

Msikilize Rais Magufuli akimsifia David Kafulila kwa kazi nzuri aliyofanya.

Comments

comments

Shares